Kocha Jurgen Klopp ameamua kufunguka kwa mara ya kwanza wakati huu akihusishwa na kibarua cha kwenda kuinoa Timu ya Taifa ya Ujerumani.

Kocha huyo wa Liverpool mara kwa mara jina lake limekuwa likitajwa na kuhusishwa na kibarua cha kuinoa Ujerumani, ambayo kwa sasa ipo chini ya Hansi Flick, huku mambo yakiwa hovyo baada ya kushinda mechi nne kati ya 16 za mwisho.

Presha imezidi kupanda kwa Kocha Flick, kutokana na Ujerumani kuwa mwenyeji wa Euro 2024 na kuna mambo mengi yanayonekana yanakwama.

Kocha Klopp ni kipenzi cha mashabiki huko Ujerumani na wanaomba hata aende akaionoe timu ya taifa kama deiwaka wakati akiendelea na ajira yake huko Anfield.

Lakini, Klopp amepuuzia uwezekano huo wa kwenda kuwa kocha wa muda huko Ujerumani, huku akisema hata maofisa wenye mamlaka kwenye soka la Ujerumani hawajampelekea ombi lolote.

“Shida ni kwamba hivi vitu vimesimama kwenye uaminifu wangu,” amesema

Klopp na kuongeza. “Siwezi kuondoka Liverpool kwa sasa na kwenda kuchukua kazi ya kuinoa Ujerumani kwa muda. Hicho kitu hakipo. Na hata maombi yenyewe sijaletewa.”

Mkataba wa sasa wa Klopp huko Liverpool utafika tamati 2026, lakini mwenyewe anajiona kabisa anakwenda kuwa kocha wa Ujerumani kwa miaka michache ijayo akisema: “Kibarua cha kuinoa timu ya taifa ni heshima kubwa. Hilo halina mjadala.”

Miquissone, Onana waandaliwa dozi maalum
CAF: Azam FC yapelekwa Ethiopia, Singida FG Zanzibar