Matumizi ya bidhaa za chuma Nchini yameongezeka kutoka Tani 226,000 hadi kufikia tani 1000,000 sawa na ongezeko la asilimia 303.54 kwa mwaka 2020 hadi 2022.
Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Julai 25, 2023 jijini Dodoma, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema Machi 2023 Nchi ilikuwa na viwanda 25 vya kuzalisha chuma na bidhaa za chuma.
“Viwanda hivyo vipo katika makundi mbalimbali yanayojumuisha bidhaa zikiwemo nondo, mabomba, misumari na senyenge na katika hivyo viwanda vya kuzalisha nondo ni tani 16 vyenye uwezo uliosimikwa kuzalisha tani 1,082,799 kwa mwaka na uzalishaji halidi ni tani 750,000 kwa mwaka sawa na asilimia 69 ya uwezo uliosimikwa,” amesema Dkt. Kijaji.
Hata hivyo, amesema “mahitaji ya nondo Nchini kwa mwaka ni Tani 550,3336 hivyo uzalishaji wa ndani unajitosheleza mahitaji yote ya ndani na ya ziada, tunajitosheleza kwa mahitaji yote na kiasi cha tani 199,664 tumeamua kuuza nje ya Nchi , hivyo tunapiga hatua na tunaendelea kupiga hatua katika uzalishaji huu,” amesema Dkt. Kijaji.
Hata hivyo, ameongezea kwa kipindi cha julai 202 hadi juni 2023 wastani wa bei ya nondo nchini ilikuwa ni shilingi 25,098 , huku mwezi Agosti 2022 ukiwa na bei ya juu kuliko miezi yote kwa shilingi 31,500.