Kocha Mkuu wa Chelsea, Mauricio Pochettino, anaamini Levi Colwill anaweza kuwa mmoja wa mabeki wa kati wakubwa nchini England baada ya mchezo wake mzuri wa kujiandaa na msimu dhidi ya Brighton.

Beki huyo mwenye miaka 20, alicheza dakika 81 za ushindi wa ‘The Blues’ wa 4-3 dhidi ya Seagulls katika mechi ya kujiandaa na msimu mpya 2023/24.

Colwill alitumia msimu uliopita kwa mkopo kule Brighton, ambapo alicheza mechi 22 katika mashindano yote na kuongeza sifa yake kama mmoja wa watu wanaotarajiwa kuimarika zaidi katika taifa lake.

Beki huyo pia aliisaidia Timu ya Taifa ya Vijana ya England kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 21.

Alipotakiwa kutoa mawazo yake kuhusu Colwill baada ya ushindi kwenye Uwanja wa Lincoln Financial, Pochettino alisema: “Levi amekuwa na siku chache mazoezini na nadhani yuko karibu kuwa fiti. Kwa kweli, kwa nini tunacheza naye ni kwa sababu tunahitaji kugawana dakika na wachezaji tofauti na nadhani yuko katika hali nzuri.”

“Nimefurahishwa naye, uchezaji wake ulikuwa mzuri. Bora kuliko nilivyotarajia kwa sababu ni mechi ya kwanza tu kwetu baada ya msimu na Brighton,” alisema Pochettino.

Colwill alijiunga na Chelsea mwaka 2011 na ameendelea kupitia mfumo wa vijana wa klabu hiyo, ingawa bado hajaonekana kwenye kikosi cha kwanza katika mechi ya ushindani.

Amecheza mara 26 kwenye kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21, akifunga mara moja dhidi ya Manchester City.

Lakini baada ya Kalidou Koulibaly kuondoka Stamford Bridge na Wesley Fofana na Benoit Badiashile wote wakiwa wamejeruhiwa, mchezaji huyo wa zamani wa Huddersfield sasa anaonekana kuwa tayari kucheza mara kwa mara pamoja na beki mkongwe wa kati, Thiago Silva.

Emmanuel Dikongue ni suala la muda tu
Azam FC kuzikabili Stade Tunis, Club Africain