Kikosi cha Maafande wa Jesho la Magereza ‘Tanzania Prisons’ chenye maskani jijini Mbeya, leo Jumatano (Julai 26) kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kombaini ya mkoani Songwe.

Akizungumza na kutoka jijini Mbeya, Msemaji wa timu hiyo, Jackson Mwafulango, amesema mchezo huo ni mwendelezo wa michezo yao ya kirafiki ikiwa ni maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 15, mwaka huu.

“Mchezo huo ni maandalizi kuelekea msimu ujao ambao tunaamini utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na usajili uliofanywa na timu zote,” amesema Mwafulango.

Amesema Jumapili ya juma hili (Julai 30) atatoa taarifa rasmi ya wapi wanakwenda kuweka kambi yao ili mashabiki pamoja na wadau wa Prisons wafahamu kile kinachoendelea.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fred Felix Minziro, amesema maandalizi yanaendelea vema kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Azam FC kuzikabili Stade Tunis, Club Africain
Kylian Mbappe, Al Hilal kukaa meza moja