Wajumbe wa Mkutano wa Askari Polisi wa Kike wa Duniani Ukanda wa Afrika IAWP, wameendelea na mafunzo yenye mada mbalimbali wakifundishwa namna ya kukabiliana na wahalifu wanaojihisha na utakatishaji wa fedha Duniani.
Akitoa taarifa hiyo hii leo Julai 26,2023 Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP David Misime amesema mafunzo hayo yanatolewa na wawezeshaji kutoka ndani na nje ya Nchi, ambapo wamefundisha mada za mikakati ya mawasiliano, uongozi, utakatishaji wa fedha na ugaidi.
Kwa upande wake, Kamishna wa Polisi, Elice Mapunda-Mstaafu ambaye ni mwanamke wa kwanza wa cheo cha Kamishna wa Polisi amesema wao kama waanzilishi wa mtandao wa Polisi wa kike Tanzania, TPF-net na kuunganishwa Jumuiya ya IAWP kuwa wajumbe wa kudumu, kitendo kilichofanikisha utekelezaji wa majukumu ya Polisi.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi SACC, Dkt. Noelia Myonga kutoka ofisi ya kiunganishi TANAPA Dodoma amesema mafunzo hayo yamewajengea uelewa katika kutekeleza Majukumu yao.