Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kujiuliza kama Bara walilolirithi kutoka kwa Waasisi waliotafuta Uhuru wa Afrika ndilo Bara wanalotaka kuwarithisha vizazi vijavyo au Wajukuu zao na kusema wakipata majibu watalijenga Bara la Afrika vizuri.

Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo hii leo Julai 26, 2023 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu Jijini Dar es salaam na kudai kuwa umakini unayhitajika ili kutoongeza idadi ya Vijana wasio na ujuzi wasioajirika na wa kujiingiza kwenye vitendo viovu na uvunjifu wa amani.

Amesema, Afrika ni Bara lenye Watoto na Vijana wengi, na hali hiyo inaweza kuwa nzuri na yenye tija endapo watawekeza kwenye rasilimali Watu kwa kuhakikisha uwepo wa afya bora, elimu bora yenye stadi za maisha ili kujenga nguvu kazi yenye tija kama wenzetu wa Bara la Asia.

“tusipofanya hivyo tutaongeza idadi ya Vijana wasio na ujuzi wasioajirika na wa kujiingiza kwenye vitendo viovu na uvunjifu wa amani, sisi tulio hapa tujiulize Bara tulilolirithi kutoka kwa Waasisi wetu waliotafuta Uhuru wa Afrika ndilo Bara tunalotaka kuwarithisha vizazi vijavyo au Wajukuu zetu, je, Afrika tunayoijenga leo ni yenye uchumi endelevu au uchumi unaodumaa?, tukipata majibu hayo tutalijenga Bara letu vema zaidi,” amesema Rais Samia.

Viongozi wa Dini wahimizwa utoaji wa elimu lishe
Robertinho: Ninaridhishwa na kikosi changu