Mwenyekiti wa Tawi la Simba Kijiji cha Mchombe kata ya Mngeta Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, Benson Mwakasanga ameuawa na watu wasiojulikana shambani Kwake kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Morogoro ACP. Hassan Omary amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Julai 25, 2023 wakati marehemu akivuna mazao shambani kwake na alivamiwa na watu hao na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.

Mwenyekiti wa Matawi ya simba Mkoa Morogoro, Saidi Mkwinda amesema club hiyo inashirikiana na ndugu wa marehemu kusafirisha msimba kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi na kudai bado haifahamika sababu za tukio hilo.

Mkoa wa Morogoro umekuwa ukikubwa na matukio ya vifo vya watu kuuawa na watu wasiojulikana ambapo katika mtaa wa Fungafunga kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro, mtu mmoja mwanaume ambaye jina lake halikufahamika alikutwa mefariki huku mwili wake ukielea kwenye dimbwi la maji.

Ongezeko la kodi: Wananchi waivuta shati Serikali
Mexime aishtukia Ligi Kuu, kuhamia Uganda