Watu wawili wamefariki papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya Basi walilokuwa wakisafiria kujaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua hatahadhari na kisha kugongana na Lori la mizigo eneo la Mkuza lililopo Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema ajali hiyo imetokea Julai 26, 2023 majira ya usiku katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro na ilihusisha Basi la Saratoga lenye namba za usajili T370 DHA aina ya Higer lililokuwa likiendeshwa na Dereva Ammy Anuru na liligongana na Lori aina ya Howo lenye namba za usajili T. 925 DRH lenye tela namba T 560 BLA.

Amesema, “Basi la abiria Saratonga lilikuwa likitolea mkoani Kigoma kuelekea Dar Es salam liligongana na gari hiyo ya mizigo ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salam kwenda Morogoro likiendeshwa na Dereva Hussein Hassan (37) na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo.”

Aidha, Kamanda Lutumo amewataka waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Dereva wa basi hilo Ammy Anuru (37), na kijana mwingine wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25 huku waliojeruhiwa ni Mnili Mohamed (36), Shabani Bomeka na Amani Jonathan.

Vituo vitapata Mafuta bila kuchelewa - TAPSOA
JKCI kuanzisha huduma uzibuaji mishipa ya uume