Kufuatia kuondoka kwa Mshambuliaji hatari kutoka DR Congo,  Mshambuliaji mwenzake Kennedy Musonda amefunguka kuwa ana kazi kubwa ya kuhakikisha anaziba nafasi ya nyota huyo kwa kupachika mabao zaidi.

Mayele raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), alimaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 17, ameondoka Young Africans na kujiunga na klabu ya Pyramids ya Misri.

Musonda raia wa Zambia, amesema ana kazi ya kuhakikisha anawafurahisha mashabiki wa timu hiyo kwa kufunga mabao katika kila mchezo msimu ujao.

“Nitahakikisha natumia vema kila nafasi ambayo nitapata nitakapopewa nafasi ya kucheza msimu ujao, ninaamini mashabiki wa Young Africans wataendelea kufurahia kila siku,” amesema.

Musonda amesema kwa kushirikiana na wenzake anaamini watafanya vizuri na kuhakikisha pengo la Mayele halionekani kwa sababu kila mchezaji ataipambania timu yake.

Musonda Alijiunga na Young Africans, mwezi Januari, mwaka huu, akitokea klabu ya Power Dynamos ya Zambia na amesaini kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

Young Africans ndiyo klabu ya kwanza kwa Musondo kucheza soka la kulipwa, tangu mwaka 2015 alipoanza kucheza mpira.

Carlo Ancelotti ampotezea Kylian Mbappe
Bayern Munich yapiga hatua kwa Harry Kane