Wauguzi wa kada ya Utabibu, Wakunga na Wauguzi wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri bila kwenda kinyume na maadili ya fani yao, na kuacha kutumia lugha chafu na kejeli kwa wagonjwa ili kuheshimisha kada hiyo.

Wito huo, umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Adolf Ndunguru kwa wahitimu 106 wa mahafali ya 56 wa taaluma ya utabibu na uuguzi, katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha, Mkoani Pwani.

Amesema, “Fani hii inazingatia maisha na uhai wa binadamu ambao haufidiwi na chochote, mmepewa dhamana kubwa kulinda afya za binadamu kupitia elimu mliyoipata, hivyo epukeni uvunjifu wa sheria za nchi na msiichafue taaluma yenu mtandaoni na matumizi ya lugha zisizo na staha kwa wagonjwa.”

Aidha, Ndunguru aliwataka kutumia mitandao ya kijamii kupata maarifa na kupanua wigo wa kutoa huduma bora za kiafya huku akisisitiza kutumia weledi unaozingatia taaluma badala ya kutekeleza wajibu wao kwa maslahi ya fedha.

Robertinho afurahia uwezo Simba SC
Carlo Ancelotti ampotezea Kylian Mbappe