Uongozi wa Mtibwa Sugar umeanza kushusha vyuma vya kazi kwa ajili ya msimu mpya 2023/24, ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ni Pascal Kitenge, Issa Rashid (Baba Ubaya) na Casian Ponera hawa hawatakuwa ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar msimu wa 2023/24.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa msimu mpya watakuwa na kikosi imara kitakachokuwa na maingizo mapya ya wachezaji bora.

“Tunafanya usajili makini na tuna vijana ambao tutawapandisha kutoka kwenye timu yetu ya U 20, hapo wapo kama sita hivi watacheza timu ya wakubwa.

“Wapo wachezaji wapya ambao tutakuwa nao kwenye kikosi ikiwa Juma Luizio, Kelvin Nashon, Mohamed Kassimu Ally na Omar Ally Marungu huyu ilikuwa ni kutoka U 20,” amesema Kifaru.

Mtibwa imeweka kambi Morogoro na inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.

RB Leipzig yaichorea mstari Man City
Manchester United yamrudia Rasmus Hojlund