Klabu ya Manchester United imeendelea kufanya mazungumzo na Fiorentina kuhusu uwezekano wa kuipata huduma ya kiungo wa Morocco, Sofyan Amrabat mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha hili ambapo taarifa kutoka tovuti ya 90min zinadai kwamba wamefikia kwenye hatua nzuri.

Amrabat ambaye ameonyesha kiwango bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana akiwa na timu ya taifa ya Morocco anadaiwa kufanya mazungumzo binafsi na kocha wa Man United, Erik Ten Hag ambaye amemuelezea kwa kina mipango yake.

Baada ya kikao hicho kiungo huyu ameonekana kuvutiwa zaidi na mipango ya Man United na ameshakubali kuvaa jezi ya mashetani hao wekundu lakini kinachokwamisha dili ni makubaliano baina ya mabosi wa Man United na Fiorentina kuhusu kiwango cha ada ya uhamisho.

Mkataba wa sasa Amrabat ambaye pia aliwahi kuhitajika na Barcelona kwenye dirisha lililopita la majira ya baridi unamalizika Juni 30, mwakani lakini una kipengele cha klabu yake kumuongeza mwaka mwingine mmoja zaidi.

Kwa mujibu wa Transfermkt, Man United ina asilimia 39 za kumpata Amrabat wakati klabu ya Al Ahly ya Saudi Arabia ambayo pia inamhitaji ina asilimia 43 za kuinasa saini ya mkali huyo.

Ihefu FC yafunga usajili 2023/24
Abdul Mingange akaribia Mbeya City