Mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani, amejiunga na Boca Juniors baada ya kusitishwa kwa mkataba wake na klabu ya Ligi Kuu Hispania, La Liga, Valencia, klabu hiyo ya Argentina imetangaza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, ametia saini mkataba wa miezi 18, huku Boca ikiomba muda wa ziada kutoka kwa FA ya Argentina ili kumsajili mshambuliaji huyo kwa hatua ya 16 ya Copa Libertadores (Ligi ya Mabingwa Amerika Kusini).

“Tumefurahi kuwa na Cavani nyumbani,” klabu hiyo yenye maskani yake Buenos Aires iliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, pamoja na video ikimkaribisha mchezaji huyo.

Cavani, ambaye alianza maisha yake ya soka akiwa na Danubio ya Uruguay, alihamia Ulaya mwaka 2007 alipojiunga na Palermo.

Baada ya misimu minne alihamia SSC Napoli, ambako alifunga mabao 104 katika michezo 138 na kushinda Coppa Italia.

Mwaka 2013, alisajiliwa na Paris Saint-Germain, ambapo alicheza kwa miaka saba, na kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu rekodi ambayo alishikilia hadi msimu uliopita wakati fowadi wa Ufaransa, Kylian Mbappe alimpita kwa kufunga mabao 212 katika mashindano yote.

Alishinda mataji sita ya Ligue 1, mataji matano ya Ufaransa na mataji sita za ligi jijini Paris pamoja na medali ya washindiwa pili katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Cavani alijiunga na Manchester United mwaka 2020 kabla ya kuhamia Valencia kwa uhamisho wa bure miaka miwili baadaye. Klabu hiyo ya Hispamia ilikubali mapema Jumamosi kusitisha mkataba wa mshambuliaji huyo, ambao ulikuwa unamalizika mwakani.

Cavani amecheza mechi 136 na kuifungia Uruguay mabao 58 na kuwa mfungaji bora wa pili nyuma ya Luis Suarez.

Aliisaidia nchi yake kushinda taji la Copa America mwaka 2011.

Hospitali ya Muhimbili yapitishwa CAF
Mrithi wa Mayele atoa kauli ya kibabe