Dili la Mshambuliaji Thomas Ulimwengu la kujiunga na Singida Fountain Gate, limetiki kwa mabosi wa klabu hiyo kumpa mkataba wa miaka miwili ukiwa na masharti ya kuongezewa kutegemeana na kiwango atakachoonyesha.

Nyota huyo aliyewahi kuwika TP Mazembe kisha kucheza JS Soaura na Al Hilal tayari amejiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo mjini Singida kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya na utambulisho utakaofanyika keshokutwa Jumatano (Agosti Pili) kwenye tamasha la ‘Singida Big Day’, litakalofanyika mjini Singida.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza kuwa, kandarasi ya nyota huyo inaweza kuongezeka ingawa itategemeana na kiwango chake atakachokionyesha pindi atakapocheza.

“Ni mchezaji mzuri tunayeamini atatusaidia, lakini mkataba huu umekuwa na masharti kidogo kwake kwa kuhofia kiwango chake kwani hajacheza muda mrefu,” kimesema chanzo chetu, huku Kocha Hans Pluijm akisema usajili wao wote walioufanya umezingatia michuano wanayoshiriki ikiwamo Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Msimu ujao utakuwa mgumu na wenye ushindani kwani kila timu inaonekana wazi imejipanga vyema kuanzia maandalizi na usajili hivyo nasi kama sehemu hiyo lazima tuonyeshe ubora wetu.”

KMC FC yamfungulia njia Majogoro
Musonda atabiriwa makubwa 2023/24