Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax anatarajia kufungua rasmi Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kushiriki katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano – JPC, kati ya Tanzania na Algeria ngazi ya Mawaziri.

Dkt. Tax anatarajia kufanikisha matukio hayo hii leo Agosti 2, 2023, baada ya kuwasili Jijini Algiers nchini Algeria kwa ziara ya kikazi ambapo alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Ahmed Attaf ambapo pia walifanya mazungumzo.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisi za Wizara jijini Algiers, Algeria Viongozi hao Dkt. Tax na Waziri Attaf wameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia, uliopo kati ya Tanzania na Algeria.

Algeria na Tanzania zinashirikiana katika sekta za nishati, elimu, afya, utalii, utamaduni, Sanaa na michezo, ulinzi na usalama, siasa na diplomasia, biashara na uwekezaji na nishati.

Sabilo kuvaa gwanda JKT Tanzania
Chirwa aongeza mzuka Kagera Sugar