Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amefungua Kikao kazi cha kupokea maoni ya wadau wa Sekta ya Madini kuhusu mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria ya Madini Sura Namba 123, pamoja na baadhi ya Kanuni zake.

kikao hicho, kitakachoendeshwa kwa siku tatu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere – JNICC, jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini nchini.

Amesema, “tuliona tusijifungie wenyewe ofisini kutengeneza Sheria tukaamua kuwaita wadau wa sekta hii ili mtoe mapendekezo yenu yatakayosaidia kurekebisha Sheria ya Madini Sura namba 123 na Kanuni zake ili kuboresha utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Madini.”

Pamoja na Mambo mengine, Dkt. Biteko ameyataja maeneo yanayohitaji kuboreshwa kuwa ni pamoja na Kanuni ya Masoko ya Madini, Kanuni ya Eneo Tengefu la Mirerani, Kanuni ya Uchenjuaji Madini, Kanuni ya Haki Madini.

Maeneo mengine ni Kanuni ya Uongezaji Thamani Madini na mapendekezo ya Kanuni mpya ya Uchenjuaji Mdogo wa Madini ili kuboresha shughuli za Sekta ya Madini na kurejesha Minada ya Madini ya Vito.

John Noble aipa jeuri Tabora United
Xhaka afichua kilichomng'oa Arsenal