Baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, kutangaza bei mpya za mafuta ya Petroli kupanda kwa shilingi 443, Dizeli kwa shilingi 391 kwa Dar es Salaam, pia zimetajwa sababu zilizopelekea ongezeko hilo kuwa ni kutokana na changamoto za kupanda kwa thamani ya Dola Duniani.
Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa leo na EWURA, Petroli iliyokuwa inauzwa shilingi 2,736 sasa itauzwa kwa shilingi 3,199 na Dizeli iliyokuwa inauzwa shilingi 2,544 ielekezwa kuuzwa kwa Shilingi 2,935, kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha EWURA imesema sababu za kupanda kwa bei hizo pia kumechangiwa na mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.
Hata hivyo, EWURA imesema Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta kwa bei ya ushindani isipokuwa zisizidi bei kikomo au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2023.