Klabu ya Manchester City imekubali kufanya mazungumzo ya mwisho na RB Leipzig ili kufanikisha usajili wa beki Josko Gvardiol, vyanzo vimeiambia ESPN.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu England wamepanga kulipa ada ya Euro milioni 90 moja kwa moja, na makubaliano hayo hayajumuishi nyongeza.

Gvardiol mwenye umri wa miaka 21 atafanyiwa uchunguzi wa kiafya na anatarajiwa kusafiri hadi England mara moja.

Kuna uwezekano mkubwa wa kucheza mechi yake ya kwanza katika Ngao ya Jamii keshokutwa Jumapili (Agosti 06) dhidi ya Arsenal huko Wembley, lakini anafaa kusajiliwa kwa wakati ili kupatikana kwa mechi ya ufunguzi wa ligi ya City dhidi ya Burnley pale kwenye uwanja wa Turf Moor, Agosti 11.

Hapo awali Leipzig walikuwa wamemtathamini Oisha Gvardiol kwa Euro milioni 100, msimamo ambao ulizuia mazungumzo mapema msimu huu wa joto.

Thamani ya Leipzig ingemfanya Gvardiol kuwa beki ghali zaidi duniani, lakini ada ya mazungumzo ya City ni chini ya Pauni Milioni 80 ambayo Manchester United ililipa Leicester City kwa Harry Maguire mwaka 2019.

Gvardiol atakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Pep Guardiola majira haya ya joto baada ya kuwasili kwa Mateo Kovacic kutoka Chelsea.

Ilkay Gündogan na Riyad Mahrez wote wameondoka, na bado kunaweza kuwa na wachezaji wengine wanaomaliza muda wao, wakiwemo Bernardo Silva, Kyle Walker, Kalvin Phillips na Aymeric Laporte.

Elimu kwa Umma masuala ya Muungano yahamia Mbeya
Usajili wa Ngoma Simba SC pasua kichwa