Huku kikosi chake kikiendelea na maandalizi ya kabla ya msimu ‘pre Season’ kwenye kambi yao ya AVIC Town Kigamboni, Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amewatuliza Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kwa kusema kuwa kikosi chake kitatetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Young Africans kwa msimu wa pili mfululizo ndiyo mabingwa watetezi wa mataji matatu makubwa ya mashindano ya ndani ambayo ni Ngao ya Jamiii, Kombe la Shirikisho la Tanzania Bara ‘ASFC’ na Kombe la Ligi Kuu Bara.

Mataji hayo Young Africans iliyatwaa katika kipindi cha misimu miwili ya utawala wa aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Mtunisia, Nasreddine Nabi ambaye alitangaza kutoendelea na klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.

Akizungumza kuhusiana na maendeleo ya kikosi chake, Gamondi amesema: “Tumekuwa na wakati mzuri wa maandalizi ya kikosi chetu kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23 na baadhi ya michezo ya kirafiki ambayo tumefanikiwa kucheza imetupa mwanga wa wapi pa kuanzia.

“Tunafahamu utakuwa msimu mgumu kutokana na mabadiliko makubwa ambayo yamefanyika kwenye timu lakini niwahakikishie Wanayanga kuwa wana kikosi bora ambacho kitapambana kutetea mataji yote tunayoshilkilia na kwa umuhimu mkubwa ubingwa wa ligi.”

Hauwezi kununua Bandari, tusikatae uwekezaji huu - Karamagi
SKUDU: Tutaipasua Azam FC mapema tu