Uongozi wa Simba SC umebainisha kuwa kiungo mpya Fabrice Ngoma ana balaa akiwa uwanjani kwa kufanya kazi tatu kwa wakati mmoja akitimiza majukumu yake.

Ahmed Aly, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema, kuwa kiungo huyo atawapa burudani Wanasimba kwenye mechi zote atakazocheza.

“Hapa ninataka kumgusia kidogo tu Fabrice Ngoma huyu ana balaa akiwa uwanjani, anacheza kisha anatoa maelekezo wa wenzake, halafu ana uzoefu mkubwa wa mechi za kitaifa na kimataifa umeona tulivyopata mchezaji mzuri.

“Kuwa na Ngoma ni mwanzo tu, anapocheza anampa maelekezo Mzamiru Yassin kisha nenda pale pasi inakuja na akisema hivyo ni uhakika pasi inafika na anatuliza timu burudani zinakuja Wanasimba watafurahi.

“Ameicheza AS Vita ile yenyewe yamoto kabisa ambayo Simba SC tuliifunga, amecheza Raja Casablanca hivyo ana uwezo mkubwa na hadhi ya kuwa ndani ya Simba SC hcbu fikiria katikati una Sadio Kanoute una Mzamiru Yassin, una Onana “unadhani nini kitatokea?” amesema Ally.

TARI yadhamiria kuondoa changamoto zao la Ngano
Kapombe, Tshabalala waahidi burudani Simba Day