Baada ya kusafisha kikosi kwa kuachana na baadhi ya wachezaji huku wakishusha majembe mapya ya kazi, Uongozi wa Kagera Sugar umesema msimu huu wana jambo lao kwenye Ligi Kuu kwani wanataka kumaliza ndani ya nafasi tano za juu.

Kagera Sugar yenye maskani yake mjini mkoani Kagera baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita ikikamata nafasi ya l1 kwenye msimamo wa ligi, iliamua kuachana na wachezaji wake wanane ambao ni Lauent Alfred, Yusuph Mhilu, Jackson Kibirige, Abeid Athuman, Yusuph Dunia, Meshack Mwamita na Erick Mwijage.

Baada ya kuwapa mkono wa kwaheri nyota hao, klabu hiyo ikaanza kushusha vyuma vipya saba hadi sasa ambao ni mawinga, Gasper Mwaipasi na Obrey Chirwa, washambuliaji Abiudy Mtambuka, Dickson Gidion, viungo Cleophas Mkandala, Richardson Ng’ondya na Ally Nganzi wote wakisaini miaka miwili kukipiga klabuni hapo kuanzia msimu ujao.

Tayari wamecheza mechi mbili wakianza kwa sare ya l-1 na JKT Tanzania Julai 29, mwaka huu katika Uwanja wa Fresho Complex mkoani Shinyanga, kisha Agosti 2, 2023 wakapoteza mabao 2-1 dhidi ya Vipers katika Uwanja wa St. Marrys.

Minziro matarajio kibao Ligi Kuu 2023/24
Dili la Lukaku bado kizungumkuti