Serikali nchini, imesema ipo tayari kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye vyombo vya juu, ngazi ya Umoja wa Mataifa sekta ya utalii kutokana na dhima ambayo Tanzania imepewa na Bara hili katika Mkutano wa Utalii Kanda ya Afrika uliomalizika hivi karibuni nchini Maritius.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema hatua hiyo inatokana na Tanzania kuchaguliwa kuiwakilisha Afrika katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani – UNWTO, na nafasi ya ujumbe katika Kamati ya Utendaji, hivyo inajipanga kuzitumikia nafasi hizo.

Amesema, “tangu tuliporejea tumefikisha rasmi taarifa hizi kwa Mhe Waziri wetu Mhe. Mohamed Mchengerwa na yuko tayari kuanza kuiwakilisha nchi na Bara la Afrika katika nafasi hizo muhimu alizoteuliwa,”

Kwa upande wao Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, TTB, Damasi Mfugale na Kaimu Mkurugenzi wa Utalii Wizarani Dkt. Theresa Mugobi, wamesema wamejifunza mambo mengi ikiwemo namna nchi zinavyopigania maslahi yao katika mikutano ya kimataifa na kubadilishana ujuzi katika kuendeleza na kutangaza utalii.

Young Africans yapongezwa usajili wa Maxi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 6, 2023