Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo Taifa, ndugu Juma Duni Haji, amesema kuna umuhimu wa Wazanzibari kushirikamana kuwa wamoja, ili kutengeneza hatma njema ya kizazi chao katika
kujenga ustawi wa masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Juma Duni ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho Bumbwini Makoba, wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa mikutano ya chama tokea kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa miezi michache iliyopita.

Amesema, Wazanzibar wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli wa nchi yao, na kushikamana na kuacha ugomvi na uhasama wa wenyewe kwa wenyewe ambao umewachosha Wanzanzibari kwani suala hilo hujitokeza kila baada ya uchaguzi.

Kuhusu suala la maadili, Mwenyekiti huyo amesema vijana wengi kwasasa hawana maadili na hivyo wamekosa mwelekeo na kuhimiza wananchi kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuwasaidia kuwa na mwelekeo wao mwema wa kuchangia ujenzi wao kimaisha na Taifa kiujumla.

Haya hapa malengo ya Singida FG 2023/24
Ulega awataka Wadau sekta ya Mifugo, Uvuvi kujisajili