Miamba ya Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wameiambia klabu ya Tottenham wanataka uamuzi wao juu ya biashara ya Harry Kanye kufikia mwishoni mwa juma hili, kwa kuweka wazi kama watakubali kumuuza nahodha huyo wa Uingereza ua hawataki.

Mabingwa hao wa Ujerumani wameripotiwa kutoa angalau ofa moja zaidi kwa Kane, ambapo imeripotiwa kuwa tayari Munich wamekubali masharti.

Tarehe hiyo ya mwisho ni ishara kwamba Bayern inazidi kuchanganyikiwa na hali ya sasa, ingawa haijabainika ikiwa wangejitenga na makubaliano yoyote ikiwa hayatafikiwa.

Hakujakuwa na maoni yoyote kwamba Kane atakuwa tayari kuongeza mkataba wake, kwa hivyo ikiwa mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy ataamua kumbakisha mshambuliaji huyo wa Uingereza itakuwa ni kumaliza nafasi ya mwisho ya klabu kupata pesa taslimu.

Maafisa wa Bayern walikutana na Levy mapema juma lililopita lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa.

Tottenham itafungua kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza huko Brentford mnamo Agosti 13.

Bayern wanaanza msimu wao kwa kukutana na RB Leipzig ya Ujerumani kwa Kombe la Super Cup.

Dirisha la uhamisho halitafungwa hadi Septemba Mosi, lakini inahisiwa pande zote zingependelea azimio kabla ya msimu mpya kuanza.

STAMICO yanyakua Tuzo Kampuni bora ya Madini 2023
Vijana wamekosa mwelekeo - ACT-Wazalendo