Watanzania 600 wanatarajia kupata ajira katika kiwanda cha kuchakata zao la muhogo kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China kwenye ukurasa wake wa Tweeter, imeeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa Balozi Mbelwa Kairuki, na Mwenyekiti Kampuni ya Afritech Greencrops Group, Han Ming Zhou.

Tarifa hiyo imezidi kueleza kuwa, Kiwanda cha Kampuni hiyo kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Oktoba, 2023 na kitanunua tani 300,000 za muhogo kutoka kwa wakulima nchini.

Aidha, Balozi Kairuki amekiomba kiwanda hicho pia kiwawezeshe wakulima kuongeza tija katika uzalishaji, kwa kuwapatia mbegu bora na mbinu za kilimo cha kisasa kitakachowawezesha kuzalisha hadi tani 30 kwa hekta, kama ilivyo katika mataifa mengine ulimwenguni.

Young Africans yatembeza mkwara Tanga
Rais Kagame apenyeza salamu za pongezi