Klabu ya Arsenal huenda ikalazimika kumlipa Nicolas Pepe Pauni 7.5 Milioni (Sh 23.7 bilioni) ili kuvunja mkataba wa Mshambuliaji huyo kutoka nchini Ivory Coast.

Endapo maamuzi hayo yatafanyika, basi yatamfanya Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 72 Milioni kuwa mchezaji wa tisa mwenye jina kubwa kuvunjiwa mkataba wake kwenye kikosi cha Arsenal tangu Kocha Mikel Arteta alipotua klabuni hapo.

Pepe mwenye umri wa miaka 29, ameshaambiwa hana maisha kwenye kikosi cha Arsenal baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo katika klabu ya Nice ya Ufaransa.

Tangu Kocha Arteta alipotua Emirates Stadium kuchukuwa mikoba ya Emery, Disemba mwaka 2019, Arsenal imevunja mikataba ya mastaa wakubwa kama Henrikh Mkhitaryan, Willian, Sokratis, Shkodran Mustafi, Mesut Ozil, Sead Kolasinac, Pierre-Emerick Aubameyang na Hector Bellerin.

Chama: Ni zamu yetu sasa
Jengeni utamaduni wa kuweka akiba ya Chakula - Rais Samia