Siku kadhaa baada ya kutoka kwa taarifa Neymar amewaambia mabosi wa PSG anataka kuondoka, taarifa za ndani zinadai huenda akatua kwa matajiri wa jijini London Chelsea.

Kwa mujibu wa tovuti ya RMC Sport, wawakilishi wa Neymar kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Chelsea ili kuona kama Mshambuliaji huyo anaweza kutuwa Stamford Bridge.

Neymar ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2025, anadaiwa kutaka kuondoka kwa sababu hana furaha na kubwa zaidi anaona mashabiki hawataki aendelee kuwepo jijini Paris, Ufaransa.

Mwaka huu baadhi ya mashabiki walikusanyika nje ya nyumba yake wakiandamana aondoke na wengine wakaahidi kumfanyia kitu kibaya.

Tukio la Neymar kutaka kuondoka linakuja wakati PSG wanapambana na sakata la Kylian Mbappe ambaye wanataka asaini mkataba mpya ama wamuuze na vyote hivyo amekataa.

Azam FC yatahadharishwa Tanga
Afrika iongeze thamani ya zao la Kahawa - Dkt. Mpango