Beki wa Manchester United, Harry Maguire, huenda akaendelea kusalia kwenye viunga vya Manchester United, kufuatia kukataa kujiunga na timu ambayo haitoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao 2023/24.

Maguire mwenye umri wa miaka 30, mkataba wake unamalizika mwaka 2025, na alitarajiwa kuondoka katika kipindi hiki cha dirisha la usajili lakini mustakabali wake bado upo njia panda.

Hivi karibuni nahodha huyo wa zamani wa Man Utd amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za West Ham Utd na Everton, lakini anachotaka yeye ni kucheza michuano mikubwa ya UEFA, ili kujihakikishia namba timu katika Timu ya Taifa ya England.

Kibadeni amkingia kifua Robertinho
Azam FC yatahadharishwa Tanga