Kocha wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Miguel Gamondi ni kama amempotezea kocha wa wapinzani wake wa kubwa wa Ligi Kuu Bara Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ kwa kusema hawezi kuwapa presha wachezaji wake kwa ajili ya timu hiyo kwa kuwa siyo wapinzani wao pekee katika ligi.

Gamondi raia Argentina ametoa kauli hiyo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Bodi ya Ligi kuachia ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Bara msimu huu ambapo timu hizo zimepangwa kucheza mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara Novemba 5 mwaka huu.

Gamondi amesema kuwa, hawezi kuwapa presha wachezaji wake kwa ajili ya kuwaangalia wapinzani wao hao, kwa kuwa wana timu nyingi ambazo wanapaswa kucheza nazo katika Ligi Kuu Bara na kuweza kupata matokeo yatakayopelekea wao kuweza kutwaa ubingwa.

“Suala la kuwaangalia hilo ni jambo la kawaida kwa sababu wao ni mmoja kati ya wapinzani wetu ambao lazima tutacheza nao, ila hatupaswi kuwahofia tutacheza nazo, kwä nini kuna timu nyingine ambazo hofu iwe kwa wao pekee.

“Simba kwetu ni kama wapinzani wengine, kutokana na mpango ambao tutaenda kucheza nao utakuwepo kwa wakati huo siyo kuhofia, hatuwezi kujenga timu ya kutaka kushindana na timu mmoja kwenye ligi, malengo yetu ni kushindana na kila timu ili kuweza kuchukua ubingwa wa msimu huu,” amesema Gamondi.

Kevin de Bruyne awekewa mtego Saudi Arabia
Sheikh Jassim aikaribia Manchester United