Ni wazi kuwa Saudi Pro League tayari inalenga wachezaji wakubwa zaidi kuwavuta kwenye klabu zao na sasa mchezaji anayetajwa sana kwenda huko ni Kevin de Bruyne wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City.

Jina la Bruyne linakwenda sambamba na Mo Salah na wanatakiwa kwa pesa ndefu wakati huu wa usajili wa majira ya joto.

Waarabu tayari wamebadilisha mazingira ya soka kwa kupata nyota walioimarika wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwemo mchezaji mwenza wa De Bruyne wa Manchester City Riyad Mahrez.

Tayari imewasajili nahodha wa Liverpool Jordan Henderson, Cristiano Ronaldo, Allan Saint-Maximin na N’Golo Kante.

Al-Hilal walizindua dau la kushangaza la Pauni Milioni 259 kwa supastaa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe huku kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akikiri: “Ligi ya Saudia imebadilisha soko kabisa.”

Hivyo kuna mashaka makubwa kama kweli A-Hilal watamkosa De Bruyne kwa ada ya zaidi Pauni 130 Milioni ambazo zinatajwa kutumwa Man City.

Maisha: Uamuzi wako umebeba hatma ya wengine
Gamondi aipotezea Simba SC