Wizara ya Kilimo na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Jeshi la Kujenga Taifa, wametiliana saini Mkataba wa mashirikiano katika kutekeleza mradi wa Utekeleaji na uendelezaji wa Program ya Kujenga Kesho iliyo Njema (Building Better Tomorrow, BBT).

Hati hizo za makubaliano, (Memorandum of Understanding), yamefanyika mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan huku wakilenga zaidi kuwawezesha Vijana kulima kibiashara.

Utiaji saini huo umefanyika Agosti 8, 2023 ambayo ilikuwa ni siku ya Kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane 2023, yenye Kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula”, yaliyofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.

Aidha, utiaji saini huo uliwahusisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Geofley Mweli, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele.

Makubaliano baina ya Wizara hizi mbili na JKT yanalenga pia kuwafundisha Vijana wa kitanzania ukakamavu, uvumilivu, uzalendo, moyo wa kujituma na kufanya kazi kwa bidii kupitia makambi ya Jeshi la kujenga Taifa, kabla ya kujiunga na Programu hii ya BBT, katika vituo atamizi vya kilimo, ufugaji, uvuvi na utunzaji viumbe maji.

Hata hivyo, kupitia program hii ya BBT Serikali inalenga kuwawezesha vijana kupata uzoefu, kuanzisha miradi ya kilimo, ufugaji na uvuvi kibiashara na kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa mazao boraya mifugo, malighafi ya viwanda na kuongeza fursa za ajira nchini.

Mkutano Wakuu wa Nchi, Serikali SADC ngazi ya Wataalamu waanza
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 9, 2023