Kikosi cha Coastal Union kimetamba hakuna timu itakayovuna alama kutoka katika timu hiyo kutokana na maandalizi bora waliyofanya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2023/2024.

Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara litafunguliwa rasmi Agosti 15, mwaka huu na Coastal Union watakUwa Ugenini dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Mwinyi Zahera, amesema kikosi chake kimeimarika na tayari wachezaji wake wamenesha kujengeka kutokana na kiwango walichokionyesha walipoibuka ka na ushindi wa bao 1-0, katika mechi ya kirafiki dhidi ya Singida Fountain Gate.

“Tumejipanga vizuri, ligi itakuwa ngumu kwa sababu sasa hivi ukiangalia timu nyingi zimefanya usajili mzuri,  tunataka matokeo mazuri kila mechi ya ligi. Nina wachezaji vijana ambao wataleta kitu na kufikia malengo.” amesema Kocha Zahera

Virgil van Dijk awapa ujumbe Liverpool
Chelsea yamfikiria Dusan Vlahovic