Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imebariki mchakato wa IGA ikisema malalamiko yaliyowasilishwa ya kupinga mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai, unaohusu uwekezaji katika Bandari za Baharini na Maziwa nchini, hayana mashiko.

Uamuzi huo, umetolewa baada ya hapo awali kuahirishwa na Naibu Msajili wa Mahakama, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Projest Kahyoza aliyesema “ulikuwa umepangwa kutolewa leo (Agosti 7, 2023), kwa bahati mbaya mwenyekiti wa jopo amepata dharura hivyo ameelekeza maamuzi haya yasomwe Alhamisi ya wiki hii, tarehe 10, 2023.”

Kesi hiyo ya kikatiba namba 5 ya mwaka 2023 ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na Mawakili wanne kutoka mikoa tofauto dhidi ya Serikali akiwemo Frank Nyalus, Alphonce Lusako, Raphael Ngonde, na Emmanuel Chengula.

Wanasheria hao waliofungua kesi, walikuwa wakipinga makubaliano hayo masharti ya baadhi ya ibara zake wakidai yanakiuka Sheria za Nchi za Ulinzi wa Rasilimali na Maliasili za na Katiba ya Nchi, pia wakisema yanahatarisha mamlaka na usalama wa Taifa na yaliridhiwa na Bunge kinyume cha utaratibu.

Try Again afunguka kinachowapa jeuri
Bilioni 10.99 zatumika kuboresha miundombinu ya Elimu