Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva, amethibitisha kutokea kwa tukio la kifo cha Muuguzi Ubatizo Sanga (55), wa Zahanati ya Kijiji cha Mawengi kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, anayedaiwa kupigwa na mchi kichwani kisha kubakwa na Mtoto wake Asifiwe Haule (25).

Muuguzi huyo, anadaiwa kukubwa na umauti huo Agosti 8, 2023 na mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi ambalo limesema litatoa taarifa zaidi juu ya tukio hilo huku Mkuu huyo wa Wilaya akisema usalama unaendelea kuimarishwa, kwani tukio limetokea ndani ya Familia.

Amesema, “nimeongea na Kaimu OCD ameniambia hilo tukio kwa kina na huyo muhusika tayari yupo chini ya ulinzi, usalama unaendelea kuimarishwa kwani tukio limetokea ndani ya Familia husika, kubwa kama huyu Mtu angekuwa hajakamatwa ina maana ingeweza kuleta shida kwenye Jamii.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mawengi, Renatho Kahako alisema Mtoto huyo alifanya mauaji ya Mama yake na baadaye akaibaka maiti na kwamba kijana huyo anadaiwa kuwa alikuwa amechanganyikiwa muda mrefu, na hayupo timamu.

CCM, ACT Wazalendo wapiga hatua muhimu Zanzibar
128 wawekewa Puto Tumboni, watatu wakubali yaishe