Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ujio wa msanii nyota maarufu wa filamu nchini China, Jin Dong utaifungulia milango zaidi Zanzibar kwa soko la watalii kutoka China na kuitangaza Kimataifa.

Rais Mwinyi ameyasema hayo hii leo Agosti 10, 2023 Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipokutana na msanii huyo nyota mwenye ushawishi na wafuasi katika mitandao ya kijamii zaidi ya Milioni 15 ambaye yupo Zanzibar kwa ajili ya kutengeneza filamu.

Aidha, Dkt. Mwinyi alimueleza msanii huyo kuwa Zanzibar ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo utalii wa fukwe za bahari zenye mchanga mweupe zinazovutia wengi duniani, utalii wa utamaduni , utalii wa Mji Mkongwe,utalii wa michezo, utalii wa visiwa pamoja na wa Mikutano.

Vilevile, Rais pia alimtembeza msanii huyo katika miongoni mwa vivutio vya Zanzibar ikiwemo kisiwa cha Mnemba, maeneo ya Mizingani, Forodhani pamoja na Mji mkongwe.

Wanajeshi watangaza Baraza lao jipya la Mawaziri
CCM, ACT Wazalendo wapiga hatua muhimu Zanzibar