Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameishutumu Benki ya Dunia kwa kutumia pesa kujaribu kuishinikiza Serikali yake juu ya sheria yake yenye utata dhidi ya mashoga, na kusisitiza kuwa hawahitaji kusukumwa na mtu yeyote kujua jinsi ya kutatua matatizo katika jamii yao.

Museveni aliyetia saini sheria hiyo dhidi ya mashoga, amesema Waganda watajiendeleza kwa kupewa mikopo, huku akidai inasikitisha kuona Benki ya Dunia wanathubutu kuwalazimisha kuacha imani, utamaduni, kanuni na uhuru wao kwa kutumia pesa.

Agosti 8, 2023, Benki ya Dunia ilisema Sheria ya Uganda ya kupinga ushoga kimsingi inakinzana na maadili ya Taasisi hiyo, na kwamba inasitisha mikopo kwa Taifa hilo na hakuna ufadhili mpya wa umma utakaowasilishwa kwa bodi yake ya wakurugenzi, ili kuidhinishwa kwa sasa.

Hata hivyo, Viongozi wa Uganda wanasema bado wanaendelea mazungumzo na Benki hiyo ya Dunia kuona ni namna gani wanaweza kulimaliza tatizo hilo bila kuathiri pande zote kikanuni.

Wilaya ya Mbeya yaanza utekelezazi agizo la Rais
Wanajeshi watangaza Baraza lao jipya la Mawaziri