Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kuhakikisha mifumo yote ya TEHAMA inasomana na Taasisi zinazosimamia sera hizo.

Kwa mujibu wa Taarifa ilitotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza kuwa Rais Samia ameto agizo hilo wakati wa uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya Teknolojia ya 5G iliyofanyika Tanki Bovu jijini Dar es Salaam.

Amesema, misingi imara kwenye TEHAMA na mifumo ya mawasiliano kisera, kisheria na kitaasisi itawezesha kujenga uchumi jumuishi wa kadijitali (Digital Indusive Economy), na kuinua maisha ya Wananchi mijini na vijijini.

Rais Samia pia ameongeza kuwa, uzinduzi wa Teknolojia ya 5G itarahisisha utoaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo utunzaji taarifa muhimu, ukusanyaji maduhuli ya Serikali, kutuma na kupokea fedha pamoja na biashara za mitandaoni.

Amesema kuongezeka kwa mkongo huo, pia kutatoa fursa kwa mitandao ya simu na watoa huduma wengine kuchagua mkongo wanaotaka kutumia, hivyo kuongeza ubora na kushusha gharama za Intaneti ambapo mkongo huo wa 2Afrika unaunganisha Bara la Asia, Ulaya na Afrika kwa urefu wa kilometa 45,100 na kutumiwa na zaidi ya watu Bil. 3 Duniani.

Tuchel ampigia debe Kepa Allianze Arena
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 11, 2023