Kocha wa FC Bayern Munich, Thomas Tuchel, amependekeza jina la Mlinda Lango wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga ili asajiliwe kwenye dirisha hili.

Tuchel amependekeza usajili wa Mlinda Lango huyo mwenye umri wa miaka 28,  ili akawe chaguo la kwanza wa timu hiyo wakati huu ambao Manuel Neuer atakuwa nje kutokana na majeraha yanayomsumbua.

Timu zote mbili zinadaiwa kuwa zimepanga kukutana kwa ajili ya mazungumzo zaidi ili kujadili masuala ya ada ya uhamisho na masuala mengine ya kimkataba.

Inaelezwa kwamba Tuchel ni shabiki mkubwa wa Mlinda Lango huyo ambaye amewahi kufanya kazi naye kwenye kikosi cha Chelsea wakati alipokuwa anafundisha klabuni hapo.

Kwa sasa Kepa ndio chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Chelsea hususan baada ya kuondoka kwa Eduardo Mendy aliyeuzwa kwenda Saudi Arabia.

Hata hivyo, Kepa haonekani kuwa na mpango wa kutaka kuondoka kwenye kikosi cha Chelsea na amepanga kutetea namba katika kikosi cha kwanza.

Zanetti amchana hadharani Lukaku
Maajabu ya Teknolojia 5G kurahisisha utoaji wa huduma