Romelu Lukaku amechanwa na mkongwe wa Inter Milan, Javier Zanetti akimshutumu kutokana na usaliti wake baada ya kuonyesha nia ya kutaka kujiiunga na Juventus.

Zanetti ambaye aliichezea Inter Milan mechi 858 amechukizwa na tabia ya straika huyo wa kimataifa wa Ubelgiji akidai amewasaliti.

“Lukaku ametusaliti, tumesikitika sana, tulitarajia tabia tofauti kutoka kwake kama mchezaji mwenye busara.”

Mkongwe huyo alimchana Lukaku baada ya mchezaji mwenzake wa zamani Lautaro Martinez kutoboa siri kwamba Mbelgiji huyo aligoma kupokea simu zake wakati wa majadiliano na uongozi wa Inter kuhusu hatma yake.

“Nilisikitika huo ndio ukweli, hata mimi nilijaribu kumpigia kipindi chote cha sintofahamu ya Lukaku, hakunijibu simu zangu pamoja na wenzake. Kusema ukweli hayo ni maamuzi yake, namtakia kila kheri lakini sitegemei haya kutoka kwake,” aliongeza Zanetti.

Kwa sasa Inter imemtema straika huyo na haina mpango wa kumsajili jumla baada ya mkopo wake kumalizika kutoka Chelsea. Kwa mujibu wa ripoti hata Juventus ambayo iliyopewa nafasi ya kumsajili imempotezea.

Jamie Carragher: Kuna nini nyuma ya pazia?
Tuchel ampigia debe Kepa Allianze Arena