Gwiji wa Soka nchini England Jamie Carragher ameingiwa na hofu kuhusu hatma ya kiungo wa Manchester City, Phil Foden kuelekea msimu mpya 2023/24.

Kiungo huyo kinda alitabiriwa mambo makubwa alipoanza kung’ara mwaka 2017 lakini ameanza kupitia kipindi kigumu kwa sababu mara nyingi Kocha Pep Guardiola anampiga benchi na kumpanga Jack Grealish.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Overlap kinachotangazwa na Garry Neville alisema: “Foden sio mdogo tena, miaka minne iliopita tulisema atakuja kuwa mchezaji bora wa England, lakini inavyoonekana kwa sasa Bellingham ndiye amewekwa katika daraja hilo.

Foden hachezi kikosi cha kwanza cha England wala Man City, Ilkay Gundogan na Riyad Mahrez wameondoka, Man City ilicheza Ngao ya Jamii bila ya Foden katika kikosi cha kwanza, wote tunafahamu uwezo wake, sijajua kwa nini inakuwa hivyo?”

Ahmed Ally: Mtihani tumeumaliza
Zanetti amchana hadharani Lukaku