Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amekemea kitendo cha baadhi ya wanunuzi wa Miti isiyokomaa na kutengeneza bidhaa zisizo na ubora ambazo zinachafua sifa ya Tanzania huku akisema hatamvumilia mtumishi yeyote atakayefanya kazi kwa mazoea.

Waziri Masanja pia amewataka Watumishi wa Shamba la Miti Sao hill la Wilayani Mufindi kuwa waadilifu na kutanguliza mbele uzalendo kwa kulinda rasilimali na kuwaelekeza Wahifadhi wa shamba hilo kusimamia vyema maeneo ya misitu yanayovamiwa na wananchi na kuwaondoa wavamizi.

“Tunakataza uvunaji wa miti ambayo haijakomaa.Tuendelee kuhamasisha uwekezaji wa mashamba ya miti ila uvunaji uwe unaokidhi vigezo, Serikali inatamani kushirikiana na wawekezaji tukubaliane juu ya uvunaji wa miti iliyo bora,” amesema Masanja.

Aidha, Waziri Masanja pia ameitaka Menejimenti ya shamba hilo kushughulikia suala la changamoto ya ukaguzi wa mali zinazoenda bandarini, akisema “Afisa ukaguzi ahakikishe bidhaa inayoondoka hapa ifanane na inayofika bandarini.Ukaguzi ufanyike vizuri na mzigo ufungwe vizuri.”

Matukio matano ya wizi ulioishangaza Dunia
ZFF yaziita mezani KMKM, JKU