Serikali imeanzisha mradi wa ujenzi wa minara mipya 758 kwa ajili va kupanua wigo wa mawasiliano (Coverage), itakayowanufasha Watanzania zadi ya milioni 8 kote nchini, ili kupunguza gharama za kuweka mkongo kwenye hifadhi za barabara.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya Teknolojia ya 5G iliyofanyika Tanki Bovu jijini Dar es Salaam.
Amesema, misingi imara kwenye TEHAMA na mifumo ya mawasiliano kisera, kisheria na kitaasisi itawezesha kujenga uchumi jumuishi wa kadijitali (Digital Indusive Economy), na kuinua maisha ya Wananchi mijini na vijijini.
Kuwepo kwa mirara inayopanua wigo wa Mawasiliano kutatoa fursa kwa mitandao ya simu na watoa huduma wengine kuchagua mshirika wanayetaka kumtumia, hivyo kuongeza ubora na kushusha gharama za Intaneti na mawasiliano.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aamehoji uwezekano wa kupatikana kwa Internet ya bure kwenye vituo vya Daladala, Masoko Makubwa, Vyuo Vikuu nk.