Eva Godwin – Dodoma.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira – DAWASA, imebuni ujenzi wa mifumo na mitambo midogo midogo, itakayoweza kuchakata zaidi ya lita 780,000 za majitaka kwa siku, iliyogharimu jumla ya Shilingi 25.7 Bilioni na itakayowanufaisha watu zaidi ya Milioni 1.8.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Jijini Dodoma, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Kiula Kingu amesema miradi hiyo inayojumuisha ujenzi wa vyoo vya umma 30, itasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hizi muhimu, na hivyo kuboresha usafi wa mazingira.

Mfano wa Mtambo wa kuchakata Maji. Picha ya India Mart.

Amesema, “miradi hii itasaidia wananchi kupata huduma za Usafi wa Mazingira kwa gharama nafuu karibu na maeneo wanayoishi, na Wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo wanaendelea na ujenzi mpaka muda huu.”

Aidha, Kingu ameongeza kuwa Miradi hiyo ni ya kisasa na katika mfumo itatoa gesi asilia kwa ajili ya kupikia, mbolea itakayoweza kutumika katika kustawisha bustani za miti na majani maji yatakayochakatwa yatatumika kwa shughuli za umwagiliaji, usafishaji wa barabara na mitaro au kupoza mitambo.

TCDC kuimarisha mifumo ya kisasa kidijitali
Mlinda Lango Azam FC akingiwa kifua