Beki wa pembeni Aaron Wan-Bissaka amesema alihofia maisha yake ya soka pale Manchester United yangefikia mwisho wakati akiwa nje ya timu baada ya Erik ten Hag kuteuliwa kuwa kocha mpya.

Beki huyo alikaa nje kwa miezi mitatu baada ya kuwasili kwa Ten Hag msimu uliopita wa joto na hakuanza mchezo hata mmoja kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia hapo Desemba mwaka jana.

Alipambana na kuwa chaguo la kwanza la beki wa kulia wa United katika kipindi cha pili cha msimu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alisema wakati fulani, alifikiri muda wake Old Trafford unaweza kuwa umefikia mwisho.

“Una hisia hiyo, lakini kwangu mimi huwa na imani hiyo ndani yangu ya kujiondoa katika hali kama hizo,” alisema Wan-Bissaka. “Nilikuwa na kichwa changu na nilikuwa tayari kufanya kile kinachohitajika.

“Ulikuwa wakati mgumu na kitu pekee unachoweza kufanya katika wakati mgumu ni kuendelea kufanya kazi. Niliinamisha kichwa chini kisha nikapata nafasi na kuisaidia timu.

“Unaweza kukaa tu na kulalamika juu yake na usijali, au unaweza kujaribu na nilifikiri njia bora zaidi ilikuwa kwangu kujaribu.”

Wan-Bissaka anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora kwenye Ligi Kuu England, lakini alisema amelazimika kufanyia kazi ya ziada ili kumvutia Ten Hag na kurudisha nafasi yake kwenye timu.

Anatazamiwa kwa vita nyingine ya kuwania nafasi ya beki wa kulia msimu huu akiwa na ushindani kutoka kwa mchezaji wa kimataifa wa Ureno, Diogo Dalot.

Jaribio la Wajaluo lakwama Kenya
Kituo cha Radio chafungiwa kwa mahojiano ya dharau