Makosa ya Kibinadamu, hasa tabia za baadhi ya Madereva zimeendelea kuwa kichocheo cha kutokea ajali za barabarani kwa muda mrefu nchini, licha ya wengi wao kukanusha huku takwimu rasmi zikienda kinyume na wanachokiamini.

Chanzo cha Makosa ya Binadamu, yamo makosa ya waenda kwa miguu, ulevi, wachungaji wa Mifugo, mafundi, Madereva, nk. lakini kundi la Madereva ndilo linalowajibika zaidi kusababisha kutokea kwa ajali kuliko wahusika wengine.

Takwimu za ajali zinazotolewa na Kikosi cha Usalama barabarani, ni chache zikihusisha ajali zinazotokana na kupasuka kwa tairi au ubovu mwingine mfano usukani kukatika/kuchomoka, ubovu wa barabara, Vizuizi vya njia, nk.

Lakini zinatoka takwimu za juu kuhusiana na uendeshaji wa hatari, uzembe wa Dereva, mwendokasi na Kuovateki kwa kiasi kikubwa huku takwimu za ajali za barabarani kati ya mwaka 2018 na 2022 zikieleza kuwa uendeshaji wa hatari ulisababisha ajali 496 mwaka 2018.

Aidha, uendeshaji huo wa hatari pia ulisababisha ajali 344 kwa mwaka 2019, 164 (2020), 192 (2021), 138 (2022) na uzembe wa Dereva ulisababisha ajali 1046 (2018), 816 (2019), 598 (2020), 574 (2021), 624 (2022)l.

Vilevile, mwendokasi hatarishi nao ulisababisha ajali 364 kwa mwaka 2018, 288 (2019), 272 (2020), 354 (2021), na 382 (2022), huku kuovateki kukisababisha ajali 217 (2018), 236 (2019), 97 (2020,) 59 (2021), 117 (2022).

Hata hivyo, Madereva na abiria waliofariki kwa ajali hizo kati ya mwaka 2018-2022 ni Madereva 178 kwa mwaka 2018, 153 (2019), 151 (2020), 168 (2021), 190 (2022), huku abiria wakiwa ni 707 (2018), 469 (2019), 502 (2020), 1355 (2021) na 625 (2022).

Takwimu hizi hazijahusisha majeruhi waliotokana na ajali tajwa hapo juu, ambazo zimeacha maelfu ya watu wakiwa na ulemavu wa viwango tofauti tofauti na kwa msingi huo basi utaona kuwa tabia mbovu za barabarani zina mchango mkubwa katika kusababisha ajali.

Ili tuweze kuhakikisha ajali hizi zinapungua na kutoweka kabisa, ujumbe huu ni muhimu na una maana kubwa kwa Watanzania, “BADILI TABIA YAKO BARABARANI, ENENDA KWA TAHADHARI, EPUSHA AJALI.”

@ Kutoka katika ukurasa wa RSA Tanzania – “Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.

Haya hapa malengo ya Tanzania Prisons 2023/24
Mandonga kubanwa TPBRC