Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema matayarisho ya sera mpya ya maendeleo ya Vijana Zanzibar, yamekamilika na itazinduliwa hivi karibuni ili kuanza kazi rasmi.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo hii leo Agosti 12, 2023 wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana kimataifa, na kupokea maandamano kutoka Taasisi mbalimbali za Vijana za binafsi, Serikali, Vyama vya siasa na kutembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya Maisara, Zanzibar.

Aidha, ametoa wito kwa taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Vijana na Mazingira kuendelea kuwekeza katika kuimarisha elimu na uchumi wa kijani kwa Vijana.

Rais Dkt. Mwinyi pia amesema, Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.8 kupitia wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hususani wanufaika ni vijana kwa sehemu kubwa.

Djuma Shaban bado yupo Young Africans
Haya hapa malengo ya Tanzania Prisons 2023/24