Takriban watu 80 wamefariki kutokana na moto ambao umeteketeza kisiwa cha Maui kilichopo jimbo la Hawaii nchini Marekani, hali ambayo imesababisha mamlaka kukosolewa kutokana na jinsi walivyoshughulikia maafa hayo mabaya zaidi ya asili katika historia ya nchi hiyo.

Tukio hilo linatokea wakati ambapo moto mwingine uliozuka kwenye kisiwa hicho usiku wa kuamkia Agosti 12, 2023 ukilazimisha mamia ya watu kuhamishiwa eneo la kaskazini mashariki ambalo nalo liliungua mwanzoni mwa wiki hii.

Hata hivyo, mkasa huo wa moto unatajwa kuwa ndiyo janga baya zaidi la asili katika historia ya kisiwa hicho, ukilipiku janga la tsunami lililosababisha vifo vya watu 61 mwaka 1960, baada ya mwaka mmoja tangu Hawaii ilipojiunga na Marekani.

Hata hivyo, Vikosi vya uokoaji vinaendelea na kazi ya kuokoa na kutafuta manusura kwenye magofu yanayofuka moshi katika eneo la Lahaina, huku wakazi wa eneo hilo wakiwa na mshangao mkubwa wa kilichotokea. 

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 14, 2023
Wahujumu ugawaji pembejeo wakalia kuti kavu