Klabu ya Liverpool imeachwa kwenye mataa baada ya kiungo nyota wa Southampton, Romeo Lavia, kudaiwa atatimkia Chelsea mara baada ya miamba hiyo kumalizana juu ya usajili wa nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji na The Blues itaweka mezani Pauni 55 Milioni.

Inadaiwa pia miamba hiyo ya Jiji la London, imefikia makubaliano binafsi na Lavia ambaye mkataba wake Southampton ulikuwa unamalizika mwaka 2027.

Lavia mwenye umri wa miaka 19 ameondolewa kwenye mipango ya Southampton msimu huu na hiyo ni ishara ya wazi ataondoka na lengo likiwa ni kupewa muda wa kujitafakari na kuchukua maamuzi kwani anasakwa na timu nyingi Ulaya.

Liverpool ilikuwa inamtaka Lavia ili kuziba mapengo yaliyopo eneo la kiungo baada ya kuondokewa na baadhi ya mastaa wao ikiwemo Fabinho na Jordan Henderson.

Lavia ni miongoni mwa mastaa walioonyesha kiwan-mgo bora msimu uliopita na alicheza mechi 35 za michuano yote na kufunga bao moja.

Ashikilia rekodi ya kula Duniani
Hatutarajii Wananchi kukosa Dawa Vituo vya Afya - Serikali