Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema malengo ya Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora za afya.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo hii leo Agosti 14, 2023 wakati akifungua kituo cha afya Bumbwini Makoba, kilichopo Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema hatua za awali zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora kufikia malengo ya kuimarisha miundombinu kwa kujenga hospitali za kila Wilaya, Mkoa na Hospitali ya Binguni itakayotoa huduma za uchunguzi.

Aidha, ameongeza kuwa, hatua nyingine ya Serikali pia ni kuamua kushirikiana na sekta binafsi ili zitoe huduma katika hospitali za Serikali zinazohusisha uchunguzi wa maradhi mbalimbali.

Udhalilishaji: TAMWA-ZNZ yataka uandishi wenye vigezo
Mashujaa FC watamba kukinukisha Ligi Kuu