Vyombo vya Habari vya ndani katika mji wa Amhara nchini Ethiopia, vimeripoti kuwa Ndege zisizo na Rubani za Jeshi la Taifa hilo, zimewashambulia waandamanaji na kuwauwa raia takribani raia 70.

Mashambulio hayo ya angani yameripotiwa dhidi ya Waandamanaji waliokuwa wamekusanyika katika mji wa Finote Selam, kulaani mipango ya jeshi la shirikisho kuingia katika eneo hilo.

Aidha, Jeshi na kundi la waasi la Fano wamekuwa wakikabiliana katika mapigano mazito katika mji wa Amhara katika wiki za hivi karibuni huku waasi hao wakidaiwa kukataa kuweka Silaha chini, hatua iliyopelekea Serikali ya Shirikisho kutuma jeshi kwenye eneo hilo.

Katika wiki za hivi karibuni, Wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa Fano wamekuwa wakikabiliana katika jimbo la Amhara yaliyosababisha kuondolewa kwa baadhi wa raia wa Mataifa ya kigeni, ikiwemo Taifa la Israeli, huku Shirika la haki za binadamu nchini Ethiopia – EHRC, likilaani tukio hilo.

Zahera ampa mtihani mzito Ibrahim Ajib
Juma Mgunda asogezewa Simba Queens